Mgombea kiti cha urais nchini Marekani Donald Trump amepongeza hatua ya raia wa Uingereza kujiondoa katika muungano wa Ulaya akisema “wamekomboa nchi yao”.

Amesema hayo alipowasili Trump Turnberry kwa ufunguzi wa mgahawa wa Ayrshire na ukumbi wa gofu,baada ya kufanyiwa ukarabati.

Kuna madai kuwa alinunua Hoteli hiyo kwa kima cha pesa ambazo hazikutajwa mwaka 2014.

Ufungamano wa kibiashara baina ya Scotland na bilionea huyo wa Marekani ulianza muongo mmoja uliopita alipoahidi kudumisha urithi wa mamake Mary MacLeod, aliyezaliwa Stornoway mwendo mfupi kutoka eneo la Hebrides.

Bwana Trump ambaye anasifika kwa kumiliki hoteli nyingi za kifahari pamoja na nyanja za gofu nchini Marekani pia alifungua moja ya Hoteli hizo nchini Uingereza katika jimbo la Menie mjini Aberdeenshire,mwaka 2012 baada ya mzozo juu ya mipango na masuala ya mazingira ambayo yalipingwa na wenyeji waliokataa kuhama.

Maandamano dhidi mgombea huyo wa urais wa Marekani wa chama cha Republican yanatarajiwa, kutoka kwa wale wanaomlaumu kwa ubaguzi wa rangi.

Vijana Wa Shelisheli Watua Salama Jijini Dar es salaam
Kenya Kukabiliana naKujiondoa kwa Uingereza