Baada ya kuangukia kidevu katika mchezo wa Mkondo wa Kwanza wa kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wanawake chini ya umri wa miaka 20 dhidi ya Namibia, kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania ‘Twiga Stars’ kimeondoka nchini tayari kwa mchezo wa Mkondo wa Pili.

Twiga Stars imeelekea Afrika Kusini usiku wa kuamkia leo, ambako mchezo wa Mkondo wa Pili utapigwa Jumamosi Uwanja wa Dobsonville Jijini Johannesburg.

Twiga Stars, inaelekea kwenye mchezo huo huku ikiwa na deni la kupoteza mchezo Mkondo wa Kwanza kwa mabao 2-1, jana Jumatano (Oktoba 20), Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam.

Mabao ya Namibia katika mchezo huo, yote yalifungwa na kiungo mshambuliaji wa Sevilla ya Hispania, Zenatha Goeieman Coleman dakika ya 22 na 61, wakati bao pekee la Twiga Stars lilifungwa na kiungo wa JKT Queens, Stumai Abdallah Athumani dakika ya 41.

Mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla kati ya Malawi na Zambia na atakayeshinda hapo amekata tiketi ya Morocco mwakani.

Trump kuja na mtandao wake wa kijamii
Gomes awanoa vikali Kanoute, Sakho, Nyoni