Uchunguzi uliofanywa na halmashauri ya kibiashara ya Umoja wa Ulaya nchini China umeonesha kuwa uchumi wa nchi hiyo unaopungua kasi.

Imeelezwa kuwa hilo ni suala kuu linaloleta wasi wasi kwa biashara za mataifa ya Ulaya nchini humo, ikifuatiwa na kasi ndogo ya ukuaji wa uchumi duniani pamoja na vita vya kibiashara kati ya Marekani na China.

kwa mujibu wa uchunguzi huo hali ya wasi wasi wa upatikanaji wa biadhaa duniani imesababishwa na kuzuka kwa ugonjwa wa COVID-19, na uchumi wa mataifa kadhaa umeathirika.

Hivyo basi Uchumi wa China umeonesha upunguaji wa kihistoria wa asilimia 6.8 katika robo ya kwanza ya mwaka huu kutokana na kufungwa kwa shughuli za kibiashara katika mataifa mbali mbali kutokana na janga hilo.

Wachezaji wa kigeni bado mtihani Azam FC
Wakulima wa Shayiri na Zabibu kunufaika msimu ujao wa kilimo