Uchumi wa Zanzibar umeendelea kukua, licha ya uwepo wa changamoto mbalimbali zinazoikabili Dunia za mabadiliko ya Tabianchi na kupanda kwa gharama za maisha kulikosababishwa na vita vya Ukraine na uwepo wa janga la Uviko-19.

Hayo yamesemwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi Ikulu mjini Zanzibar, katika muendelezo wa utaratibu aliojipangia wa kukutana na waandishi wa habari kila mwisho wa mwezi na kujibu maswali juu ya miaka miwili ya Uongozi wake.

Amesema, kukua huko kwa uchumi kumechangiwa na kuongezeka kwa makusanyo katika Uwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karume, ambapo sekta ya utalii imekusanya zaidi ya shilingi bilioni 6.7 katika kipindi cha kuanzia mwezi Julai hadi Septemba 2022.

Mandhari ya Kisiwa cha Zanzibar kutokea juu.

“Sekta ya Uwekezaji nayo imepata mafanikio makubwa, Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) imefanikiwa kusajili miradi 181 yenye thamani ya zaidi ya Dola Bilioni Tatu za Kimarekani na wastani wa Wananchi 11,289 wanatarajiwa kupata ajira,” amesema Rais Mwinyi.

Hata hivyo, ameongeza kuwa Serikali inakusudia kufanikisha miradi mbalimbali katika kipindi cha miaka mitatu ijayo, ukiwemo mradi wa ujenzi wa Bandari Mangapwani, barabara kuu ya Unguja na Pemba, uwanja wa ndege wa Pemba na barabara za ndani.

Ndege ya Precision Air yanguka Ziwa Victoria
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Novemba 6, 2022 Â