Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA hii leo limechezesha droo ya upangaji wa michezo ya hatua ya 16 bora ya michuano ya Europa League baada ya kumalizika kwa hatua ya mtoano hapo jana.

UEFA wamekamilisha mpango huo wakiwa kwenye makao makuu yao huko mjini Nyon nchini uswiz ambapo baadhi ya mashabiki wa soka duniani walifuatilia upangaji huo wa michezo ya hatu ya 16 bora kupitia televisheni zao.

Shughuli ya kuchezesha droo ya kupanga michezo ya hatu hiyo ilisimamiwa na katibu mkuu wa UEFA, Gian Infantino ambaye pia ni mgombea nafasi ya urais wa shirikisho la soka duniani FIFA.

Matokeo ya droo hiyo ni kwamba Tottenham wameangukiwa kwa miamba ya soka kutoka nchini Ujerumani katika ligi ya Bundesliga, Borussia Dortmund, huku klabu ya Valencia, iliyo chini ya meneja kutoka nchini England Gary Neville, wakipangwa na wapinzani wao kutoka nchini Hispania Athletic Bilbao.

Mabingwa watetezi Sevilla, ambao wametetea ubingwa wa michuano hiyo mara mbili mfululizo wamepewa FC Basel kutoka nchini uswiz na wataanzia ugenini katika uwanja wa St Jakob-Park, ambao ndio utakua mwenyeji wa mchezo wa hatua ya fainali mwaka msimu huu.

Mashetani wekundu, Man Utd wao watabaki nchini England kufutia droo iliyochezezwa hii leo kuwakutanisha na mahasimu wao wakubwa duniani Liverpool.

Droo kamili ya Europa League hatua ya 16

Shakhtar Donetsk v Anderlecht

Basel v Sevilla

Villarreal v Bayer Leverkusen

Athletic Bilbao v Valencia

Liverpool v Manchester United

Sparta Prague v Lazio

Borussia Dortmund v Tottenham

Fenerbahce v Braga

Mawaziri wa Magufuli wanusurika ‘kutumbuliwa jipu’, Ikulu yanena
Sexwale Ajiondoa Uchaguzi Wa FIFA