Mwandishi wa habari Mwandamizi kutoka visiwani Zanzibar Abubakar Kisandu, amevunja ukimya baada ya kuchukizwa na taarifa za visiwa hivyo kupokonywa uanachama shirikisho ndani ya Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’.

Kisandu ameandia taarifa inayotoa ufafanuzu wa sakata hilo ambalo jana Alhamis lilichukua nafasi kubwa kwenye mitandao ya kijamii.

Kisandu ameandika: Naomba nitowe ufafanuzi kidogo kuhusu taarifa ambazo sio rasmi za Zanzibar Vilabu vyake kukosa fursa kushiriki Mashindano ya CAF.

Kwanza hizo si taarifa sahihi (uzushi) kwa vile hakuna chanzo rasmi kutoka CAF kilichotoa hizo taarifa, wala Shirikisho la Soka Zanzibar (ZFF) hawajapokea taarifa hizo kwa njia yoyote ikiwa email, barua za kawaida hata katika simu, kwaiyo inaonyesha kuwa ni uzushi na vyombo vilivyotoa hizo taarifa watufahamishe wamezitoa wapi na hao CAF maamuzi hayo yameamuliwa katika kikao gani? ulimwengu wa sasa huko CAF sio mbali na hakuna siri mambo ya sasa ni utandawazi.

Narejea kusisitiza Zanzibar itaendelea kutoa timu Shiriki katika Mashindano ya CAF kwa Vilabu kwani mpaka sasa tayari KMKM ambao ni Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu Soka ya Zanzibar Watashiriki Mashindano ya Klabu Bingwa Afrika msimu ujao wa mwaka 2021-2022 (CAF CL) na Mafunzo ambao ni Mabingwa wa Kombe la ZFF wataiwakilisha Zanzibar kwenye Mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF CC) kwa msimu ujao wa Mwaka 2021-2022 na mpaka sasa timu hizo zimo kwenye mfumo wa Usajili wa CAF wa msimu 2021/2022.

Nenda kaangalie kwenye Website ya CAF na mfumo wa usajili timu zetu za Zanzibar KMKM na Mafunzo ni miongoni mwa vilabu ambavyo CAF wameshavipokea ushiriki wao na zoezi la usajili wa wachezaji linaendelea ambapo zaidi pia CAF wameengeza idadi ya wachezaji kwenye usajili kutoka 30 mpaka 40 kwa timu.

Nirudi nyuma kidogo Machi 16, 2017 ilikuwa ni siku ya furaha kwa Wazanzibar ambapo katika mkutano Mkuu wa CAF uliofanyika Mjini Addis Ababa nchini Ethiopia CAF lilitangaza kuwa Zanzibar mwanachama mpya kamili wa 55 wa CAF.

Lakini July 21, 2017 ni siku ya huzuni kwa Wazanzibar baada CAF kuwapokonya Zanzibar uanachama wa kudumu wa 55 wa CAF, ambapo alokuwa Rais wa CAF kipindi hicho Ahmad Ahmad alisema haiwezekani nchi moja (Tanzania) kuwa na wanachama wawili kwenye shirikisho hilo moja, hivyo uanachama huo wa Zanzibar ndani ya CAF ulidumu kwa siku 128 tu tangu Machi 16 hadi July 21, 2017.

Hivyo Zanzibar kwa sasa sio mwanachama wa kudumu wa CAF, lakini inaendelea kuwa mwanachama mshiriki (Associate Member) na ndio maana vilabu vyake vinashiriki.

RC Makalla: Abiria washushwe stendi ya Mbezi
Polisi Tanzania FC yapata ajali