Matokeo ya kura ya maoni iliyoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF baada ya kuwahoji watu 243,512 duniani kote inaonesha nusu ya vijana barani Afrika wamesema wanafikiria upya suala la kupata watoto ama la kutokana na mabadiliko ya tabianchi.

Ripoti hiyo, iliyotolewa kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP27, ambao unaondelea huko Sharm el-Sheikh Misri, imeeleza kuwa vijana wawili kati ya watano wamesema athari za mabadiliko ya tabianchi zimewafanya kufikiria upya hamu yao ya kuanzisha familia.

Vijana.

Aidha, ripoti hiyo imezidi kufafanua kuwa, “Wasiwasi huu umekuwa mkubwa zaidi katika kanda za Afrika, huku asilimia 44 ambayo ni kubwa ya vijana walioripoti kwamba wanafikiria upya kupata watoto wanapatikana Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini na asilimia 43 kutoka Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.”

UNICEF kupitia ripoti hiyo, imedhihirisha kuwa vijana katika kanda hizo mbili wameripoti kukumbwa na mshtuko na atharin za mabadiliko ya tabianchi, zaidi ya vijana wengine ulimwenguni, wakisema majanga haya yameathiri upatikanaji wao wa chakula na maji, pamoja na mapato ya familia zao.

Air Tanzania yapunguza Safari za ndege
Jeshi la Congo, waasi wa M23 waanza mapigano