Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amethibitisha kuwa moto ulizuka na kuanza kuteketeza sehemu ya Soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa, vyombo vya Serikali pamoja na wananchi walishirikiana kuuzima moto huo.

“Ni kweli soko linaungua na tuko hapa tunapambana kuuzima moto. Umeanza kama nusu saa iliyopita, tupo kwenye eneo tunapambana kuuzima,” Makalla aliliambia Gazeti la Mwananchi.

Hata hivyo, hakueleza chanzo cha kuzuka moto huo. Alisema moto huo ulianza majira ya saa tatu na nusu usiku, Julai 10, 2021.

Messi aiongoza Argentina kuichapa Brazil
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Julai 11, 2021