Wizara ya mambo ya nje ya Marekani, imesema itatoa zawadi ya hadi dola milioni 10 kwa yeyote atakayekuwa na taarifa za viongozi wakuu wa Al-Shabab huku ikibainisha kwa mara ya kwanza itatoa donge nono kwa mtu yeyote atakayewezesha kusaidia kutatiza mifumo ya kifedha ya kundi la Al-Shabab, lenye mafungamano na Al-Qaeda.

Aidha, Marekani pia imetangaza zawadi nono ya hadi dola milioni 10 kwa taarifa zozote juu ya maficho ya kiongozi wa Al-Shabab Ahmed Diriye, naibu wake Mahad Karate na raia wa Marekani anayesemakana kuwa na majukumu mbalimbali katika kundi hilo, Jehada Mostafa.

Shilingi 1.2 bilioni zimetolewa kwa taarifa zitakazowezesha kutambulishwa au kutaja eneo waanalopatikana Viongozi wa kundi la Al-Shabab Ahmed Diriye, Mahad Karate na Jehad Mostafa. Picha ya Collins Kweyu wa Standard.

Raia huyo wa Marekani, Diriye anahusishwa na shambulio la mwaka 2020 katika kambi ya jeshi nchini Kenya, lililomuua mwanajeshi mmoja wa Marekani pamoja na wakandarasi wawili ambapo awali, Marekani ilitoa zawadi ya hadi dola milioni 6 kwa yeyote mwenye taarifa kuhusu Diriye, ambaye pia anajulikana kama Abu Ubaidah.

Marekani imesema, Viongozi hao wa Al-Shabab wamehusika na mashambulizi mengi ya kigaidi nchini Somalia, Kenya na mataifa jirani na kusababisha vifo vya maelfu ya watu wakiwemo raia wa Marekani.

Wapiganaji hao wa Al-Shabab, wamekuwa wakishambulia katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu na maeneo mengine ya nchi hiyo, kujibu mashambulizi dhidi yao yanayofanywa na serikali mpya ya Rais Hassan Sheikh Mohamud.

Adel Zrane: Nipo tayari kurudi Simba SC
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Novemba 15, 2022Â