Utumbuaji sasa ni kila mahala pengine hilo ndilo linaloweza kuelezwa kuhusiana na taarifa kasi ya utumbuaji majipu imekumba pia Idara ya Mahakama ambapo mahakimu zaidi ya 60 wamejikuta wakifikishwa kortini kukabiliana na makosa mbali mbali huku wengine wakitimuliwa.

Aidha, Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kuanzia Januari hadi Desemba 2016, mahakimu 62 wamefikishwa mahakamani wakikabiliana na mashtaka mbalimbali yakiwamo ya rushwa na jinai.

“Mahakimu na watumishi wengine wa mahakama walifutwa kazi baada ya hatua zote kufuatwa, ikiwa ni pamoja na tume ya utumishi wa mahakama kujiridhisha pasi na shaka kuwa walihusika katika vitendo viovu vinavyokwenda kinyume na sheria ya utumishi nchini wakiwemo mahakimu 11 wafawidhi wa mahakama ya mwanzo, na maofisa  wa mahakama 23 kutokana na utovu wa nidhamu na maadili,”amesema Mwakyembe.

Aidha , Mwakyembe amesema kuwa moja ya mambo anayoyasisitiza na Serikali ya awamu ya tano tangu iingie madarakani ni kuongeza ufanisi katika utendaji kazi wa taasisi za umma.

Majaliwa afuta posho zote Dar
Rainford Kalaba Alikataa Soka La Ulaya