Chama cha Wananchi (CUF), kimetakiwa kuacha kufuatilia na kuhoji uhalali wa kikao cha Kamati Kuu (CC) ya Chama cha Mapinduzi( CCM) kufanya vikao vyake Ikulu kwa madai kuwa kufanya hivyo ni kutumia rasilimali za umma kwa maslahi ya chama.

Aidha taarifa iliyotolewa na Kaimu Katibu Mkuu  wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Shaka Hamdu Shaka ,kwa vyombo vya habari  jijini Dar es salaam, imesema hoja hiyo iliyotolewa na kiongozi wa CUF, Mbarara Maharagande kushutumu hatua hiyo haina mashiko.

“UVCCM tunamwambia mwanasiasa huyo, amekwenda kombo, hajui kulinganisha wala kutofautisha mambo, alichokisema ni porojo tu na hiyo taarifa aliyoiandika kwa umma haina mantiki, haikuwa na kichwa wala miguu,kiufupi haikueleweka na kufahamika alichokusudia kukisema”amesema Shaka.

Shaka amesema kuwa Viongozi mbalimbali wa Upinzani wamekuwa wakialikwa Ikulu na kutumia rasilimia hizo ikiwemo kuandaliwa chakula na vinywaji.

Aidha, amemtaka Maharagande kutumia muda na rasilimali za CUF kutatua mgogoro  uliokigubika chama chao na kuwafanya viongozi wao kutokaa meza moja.

 

Video: Dangote awaibua wasomi kwa JPM, Miili kwenye viroba yamuibua Mwigulu...
Lowassa ajitwisha shida za CUF