Mkali wa Aje, Ali kiba ameeleza sababu ya kutoonekana akifukuzia kufanya nyimbo na wasanii wenzake hasa nje ya nchi wanapokutana kwenye matamasha makubwa, kuwa sio lengo lake.

King Kiba alifunguka kwenye red carpet ya tuzo za MTV MAMA wikendi iliyopita alipofanya mahojiano na Lil Ommy, mtangazaji wa 100.5 Times Fm. Alisema kuwa hivi sasa focus yake ni kufanya muziki mzuri na sio kutafuta wasanii wa kufanya nao nyimbo.

“Hiyo sio focus yangu, focus yangu ni kufanya muziki mzuri,” alisema. “Mambo ya collaboration tutapanga kwa njia proffessionally,” aliongeza.

Ali Kiba alikuwa ametajwa kuwania tuzo ya Wimbo Bora wa Kushirikishwa kwenye tuzo hizo kupitia ‘unconditionally Bae’ alioshirikishwa na kundi la Sauti Sol. Ingawa hakushinda tuzo hiyo, alifanya show nzuri pamoja na kundi hilo.

Video: Watu 400 kufanyiwa upasuaji wa mabusha bila malipo, Ilala
Video: Waziri Mwijage asema watanzania wanapenda elimu 'mserereko', Azungumzia elimu yake