Msanii Baraka The Prince amekerwa na utani wa mchekeshaji Stan Bakora baada ya kurudia wimbo wake ambao amemshirikisha Ali Kiba  unaoitwa  “Nisamehe”.

Baraka ameonyesha kutokupendezwa na jinsi Stan Bakora alivyojipaka rangi nyeusi katika video ya wimbo huo kuonyesha kufanana naye. Hali hiyo imemfanya Baraka kushindwa kuvumilia na kutoa onyo kwa mchekeshaji huyo ambapo amefunguka kupitia ukurasa wake wa Instagram maneno haya :-  “Matani ni mazuri ila yakizidi yanaweza kuleta matatizo… heshima ichukue nafasi yake tafadhali mzee @stanbakora utani huu sijaupenda iwe mwanzo na mwisho tafadhali”

Tazama hapa video aliyoifanya mchekeshaji Stan Bakora ya wimbo wa Baraka The Prince ft. Ali Kiba – Nisamehe

Joe Hart: Torino Ni Mahala Sahihi Kwa Mchezaji Kama Mimi
Real Madrid Yaendelea Kupata Majanga