Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema kuwa kinaunga mkono kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli aliyoitoa akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Pwani kuhusu wanafunzi wa shule kupata ujauzito wakiwa bado shuleni.

Hayo yamesemwa na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Humphrey PolePole alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo jijini Dar es salaam, amesema kuwa haiwezekani mtoto kusoma katika mfumo wa mwanzo kwani akishapata ujauzito itabidi akajifungue kwanza.

“Mnajua baada ya Rais kutoa kauli hii, kuna baadhi ya watu wanajaribu kupotosha, ukweli ni kwamba Rais yupo sahihi na sisi CCM tunamuunga mkono,”amesema PolePole

Video: CCM waridhishwa na utendaji kazi wa JPM
Mbowe afafanua malalamiko yake kuhusu Lowassa kuitwa Polisi