Chama Cha Alliance For Democratic Change (ADC) kimemuomba Rais Dkt. John Magufuli kulegeza masharti aliyoyaweka katika siasa ili waweze kufanya mikutano ya hadhara ambayo itasaidia wanachama wao kujua mipango ya chama.

Hayo yamesemwa mapema hii leo jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu wa Chama hicho, Doyo Hassan Doyo mara baada ya kufanya ziara katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam. Paul Makonda.

Amesema kuwa shughuli za siasa ni haki ya kila chama kikatiba kwani kuzuia shughuli hizo ni kubinya uhuru na taratibu zilizoelekezwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha, Chama hicvho kinaadhimisha miaka mitano tangu kianzishwe kwa kufanya ziara ya kutemblea vyombo vya habari  mbalimbali vya ili kuweza kutoa ushirikiano na kujitangaza hasa katika kuelezea mafanikio waliyoyapata.

Exclusive: Vanessa afunguka anachofanya akipigwa na misukosuko, stress (Video)
Video: Tanzania na Kenya zamaliza tofauti zao za kibiashara