Kufuatia uamuzi wa aliyekua mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF Prof. Ibrahim Lipumba kuandika barua ya kutaka kurejea katika wadhifa wake wa uenyekiti.

Chama cha Wananchi CUF kupitia kwa Mwenyekiti wa Kamati ya uongozi Taifa Twaha Issa Taslima wamemuomba Prof Lipumba kutowayumbisha kwa maamuzi yake ya kutaka kurejea tena kwenye nafasi hiyo wakati awali aling’atuka.

“Chama cha Wananchi CUF kinapenda kuchukua nafasi hii kumuomba Profesa Lipumba kwamba asijaribu kukiyumbisha Chama katika kipindi hiki ambacho nchi ina matatizo makubwa ambapo Watanzania wanahitaji kuwekwa pamoja na kupewa matumaini ya namna gani matatizo yao yanaweza kutatuliwa” – Taslima

Utapenda jibu la Oprah kwa Donald Trump baada ya kumuomba awe mgombea mwenza wake
Video: Wabunge Chadema wasimamishwa kuhudhuria vikao kwa kulidanganya bunge