Mmiliki wa lebo ya muziki ya WCB, Diamond Platinumz amempongeza na kumtia moyo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa juhudi zake katika vita dhidi ya dawa za kulevya.

Akizungumza katika hafla ya kutimiza mwaka mmoja tangu Mkuu huyo wa mkoa alipoteuliwa kushika nafasi hiyo, Diamond alimtaka kutokatishwa tamaa na maneno au kwa namna anavyopingwa na baadhi ya watu bali aendelee kusimamia maendeleo.

“Unajua katika maisha, usidhani kila mtu atakipenda, ataridhika au atakifurahia unachokifanya kwa sababu kila mtu ana mtazamo wake. Cha muhimu unatakiwa kuliona hilo na kuendelea kusimamia haki na maendeleo unayotaka kuyafanya,” alisema Diamond.

Msanii huyo aliongeza kuwa hata mitume wa Mungu walipingwa na hata kufikia hatua ya kusulubiwa msalabani, hivyo ni kawaida kwa binadamu kupinga.

“Cha mwisho cha kumalizia, nataka nimwambie mkuu wa mkoa na kamati nzima inayosimamia vita hii, ukiona mtoto analia sana ujue viboko vinamkolea,” alisema.

Angalia video hii kupata alichokisema kiundani na jinsi alivyozungumzia suala la T.I.D kuacha dawa za kulevya pamoja na mpango wa kuachia wimbo waliofanya pamoja:

Bao La Ugenini Laing'oa Man City
Video: Makonda amshukuru JPM kwa kumteua kuwa mkuu wa mkoa