Wasanii wa filamu wampongeza waziri wa habari utamaduni na michezo Nape Nnauye kwa hatua aliyochukua kuhakikisha kazi za wasanii zinaheshiwa na kutaka zoezi hili la ukaguzi liwe endelevu hata katika nchi jirani.

Hata hivyo  Muigizaji maarufu ‘Mzee Chilo’ amewataka wananchi kuwa mstari wa mbele kununua kazi halisi ili kukuza sanaa na kuwapa ushirikiano waigizaji wanaofanya kazi ya kuburudisha.

Naye Kulwa Kikumba ‘Dude’ amesema zamani hakukua na uhalifu katika mikanda ya VHS lakini kwa sasa wauzaji wamekuwa waizi wanaofanya kazi mchana, hivyo wameitaka Serikali isifanye kazi ya kulinda kazi zao kwa nguvu ya soda na kuwabana wale wanaodurufu kazi za wasanii.

Vyuo Vikuu Tanzania Vyatakiwa Kuunga Mkono Uanzishwaji Viwanda
Didier Drogba: Hakuna Zaidi Ya Cristiano Ronaldo