Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini, Joseph Kasheku Msukuma amesema kuwa inauma sana kuteua wapinzani kwani mwaka 2020 hapatakuwa na upinzani imara.

Ameyasema hayo jijini Arusha alipokuwa akizungumza na Dar24 Media ambapo amesema kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitarudi kwa asilimia mia moja hivyo wapinzani hawatakuwepo.

Aidha, Msukuma amewataka wanachama waliojiunga na chama hicho kutoka upinzani na kuteuliwa na Rais Magufuli katika nyadhifa mbalimbali waende wakachape kazi.

“Inauma sana kumteua mpinzani maarufu katika wadhifa wowote, lakini mtu akishasema kuwa mimi ni mwana CCM, hakuna tatizo ana haki ya kuteuliwa,”amesema Msukuma

Chelsea yamgeukia Kepa Arrizabalaga Revuelta
NEC yavitahadharisha vyama vya siasa vitakavyokiuka utaratibu

Comments

comments