Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam limeanzisha Operesheni maalum kwaajili ya kuwasaka na kuwakamata wezi wa vifaa mbalimbali vya magari ikiwa ni pamoja na wanunuzi wa vifaa hivyo kutoka sehemu mbalimbali za jiji la Dar es salaam.

Hayo yamesemwa mapema hii leo na Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam, Lucas Mkondya alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa katika operesheni hiyo kali na endelevu, jumla ya watuhumiwa arobaini na nne wamekamatwa baada ya kukutwa na makosa mbalimbali.

Amesema kuwa watuhumiwa hao baada ya kupekuliwa walikutwa na vifaa mbalimbali vya magari ikiwemo side mirrors, taa za magari, milango ya magari, vitasa vya magari na radio za magari.

Aidha, amesema kuwa jumla ya Power Windows 69 zilizokamatwa, Radio 21, taa za magari aina mbalimbali 152, Side mirrors 105, vitasa vya magari 136, Wiper Switch 7, Air Cleaner 1, Booster na vingine vingi.

Hata hivyo, ameongeza kuwa baada ya kuwafanyia mahojiano watuhumiwa wote waliokamatwa wapo walioshindwa kuvitolea maelezo vifaa hivyo ni wapi walipovitoa  vifaa hivyo huku baadhi ya vifaa vikionyesha kuwa vimefunguliwa mahali.

Tundu Lissu akamatwa uwanja wa Ndege wa JNIA
Video: JPM awataka Warundi wote warudi kwao