Kiwanda cha kutengeneza mifuko(viroba) cha Unberg International kinachomilikiwa na Raia wa China kilichopo barabara ya Mandela jijini Dar es salaam, kimetozwa faini ya shilingi milioni 25 kwa kukiuka sheria ya mazingira ya mwaka 2004 na kanuni zake.
Hayo yamebainika katika siku ya pili ya hitimisho ya ziara ya kushtukiza ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina alipokua akikagua baadhi ya Mazingira ya jiji la Dar es Salaam na viwanda na kujionea namna ambavyo raia hao wa China wanavyotiririsha uchafu wa kinyesi cha binadamu katika mto msimbazi.
Adhabu hiyo ilitajwa na Mratibu wa Kanda ya Mashariki kutoka baraza la Taifa la hifadhi na usimamizi wa mazingira NEMC, Jafari Chimgege, ambapo amesema kiwanda hicho kinatakiwa kulipa faini ndani ya siku 7. Bofya hapa kuazama video