Waziri Mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema Serikali inataka kuwa na watumishi wanaotambua nafasi zao na watakaofanya kazi kwa uadilifu, uaminifu pamoja na uwajibikaji mkubwa hivyo kila mtu ahakikishe anafanya kazi vizuri na yenye matokeo chanya.

Majaliwa amesema kuwa kuna watu wanaona ukuu wa idara ndiyo kila kitu, hata yule anayekimbiza mafaili hathaminiwi, na kuwaabia kuwa jambo hilo si jema kwani wote ni kitu kimoja, ni watumishi wa Serikali, hivyo kila mmoja amthamini mwenzake.

“Mkurugenzi yeyote asikubali kuwa na wakuu wa Idara wasiokuwa na ushirikiano na watumishi wengine kwa sababu hataweza kupata mafanikio ya kiutendaji ndani ya eneo lake,” Majaliwa.

Danny Welbeck Kurejea Uwanjani Mwishoni Mwa Mwaka
Crystal Palace Yakubali Kumsajili Christian Benteke