Kituo cha sheria  na haki za binadamu (LHRC) leo Septemba 26, 2016 kimeadhimisha miaka 21 tangu kianzishwe mwaka 1995 kwa kutoa msaada wa vitu mbalimbali katika kituo cha watoto wanaoishi katika mazingira magumu kilichopo Kurasini jijini Dar es salaam.

Mkurugenzi wa LHRC, Bi. Hellen Kijo Bisimba amesema Serikali inatakiwa kutoa adhabu kali kwa wazazi wanaotelekeza familia zao.

Bi Simba amesema huo ni mwendelezo wa utaratibu waliojiwekea kwa kila mwaka na kutoa mapendekezo  kwa serikali kupitia wizara ya afya, ustawi wa jamii, jinsia, vijana ,wazee na watoto,  kufanyia marekebisho sheria ya watoto na kutilia mkazo malezi bora kwa watoto.

”Sisi kama kituo ni sehemu ya jamii tumekuwa tukiona ongezeko la ukiukwaji  wa haki za watoto katika jamii hali ambayo inapelekea kuwepo kwa watoto wanaokosa malezi ya wazazi au walezi na kujikuta wanaishi katika vituo vya kulelea  watoto au wakati mwingine kuishi mitaani”- Bi Simba

Majaliwa awasili Kibiti wilayani Kilwa kwa ziara ya kikazi
Podolski Amchana Mourinho, Amwambia Hana Utu