Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli ameonya kuwa kama kuna kiongozi yeyote ambaye hayupo tayari kutekeleza maagizo yake aachie ngazi mara moja na siyo kuendelea kufanya kazi kinyume na maagizo yake.

Kauli hiyo ya Rais Magufuli ni kufuatia baadhi ya Wakuu wa mikoa, Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri kuendelea kuwasumbua wafanya biashara wadogo kwa kuwahamisha maeneo yao wanayofanyia bishara na kuwalekezea maeneo ambayo hayajaandaliwa kwa ajili yao.

Magufuli amesema kitendo hicho siyo kizuri na si maagizo yake na ameeleza kukerwa na kitendo hicho, amesema kuwa anajua kero za wananchi hivyo hataki wasumbuliwe kwani kufanya hivuyo siyo kutatua matatizo badala yake ni kuyaongeza.

Hivyo, amemuagiza Naibu Waziri na Katibu Mkuu katika Ofisi ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kusitisha mara moja utekelezaji wa zoezi la kuwaondoa wafanyabiashara wadogo maarufu kwa jina la Machinga katika Jiji la Mwanza pamoja na mikoa mingine mpaka hapo mamlaka husika zitakapokamilisha maandalizi ya maeneo watakapohamishiwa na kwa kuwashirikisha wamachinga wenyewe.

Rais ametoa agizo hilo Desemba 6, 2016 akiwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, Naibu Waziri na Katibu Mkuu (TAMISEMI) Ikulu Jijini Dar es Salaam huku akionya kuwa kiongozi yeyote ambaye hayupo tayari kutekeleza agizo hilo aachie ngazi.

Aidha, Rais Magufuli ameiagiza Wizara ya Nishati na Madini kusitisha mara moja zoezi la kuwaondoa wachimbaji wadogo wa madini katika Kijiji cha Nyaligongo kilichopo katika Kata ya Mwakitolyo Mkoani Shinyanga na badala yake wachimbaji hao waachwe waendelee na shughuli zao, na leseni ya mwekezaji anayedai eneo hilo ni lake aondolewe.

Hata hivyo, Rais Magufuli amesema maagizo yake hayana maana kuwa Wamachinga na Wachimbaji wadogo waendeshe shughuli zao kwa kuvunja sheria bali wazingatie sheria na Mamlaka zisiwanyanyase watu wanyonge.

 

Professional review of Custom Writing Company with regard to College Students
Viongozi matumbo joto, ni baada ya mali zao kuanza kuchunguzwa