Usiku wa kuamkia leo Februari 7, 2021, limefanyika tamasha la Music Serengeti Festival makao makuu ya nchi, kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, likikutanisha wasanii zaidi ya 70 kwenye jukwaa moja.

Tamasha hilo linaloandaliwa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, linafahamika kama Serengeti Music Festival au Tamasha la Vipaji.

Wasanii mbalimbali walitumbuiza akiwemo mbunge wa Muheza Hamis Mwinjuma maarufu Mwana FA, ambaye aliwakosha mashabiki wake na ngoma ya Gwiji.

Pia wasanii kama Madee, Tunda Man, Nandy, Shilole, Snura, Whozu, Z-Anto na wengine wengi walipita jukwaani kutoa burudani kwa wakazi wa Dodoma na kanda ya kati kwa ujumla.

Pia Waziri wa Habari Innocent Bashungwa alikuwepo pamoja na Naibu Wake Abdallah Ulega, mbunge wa Dodoma Mjini Anthony Mavunde, mbunge wa Shinyanga mjini Patrobas Katambi na wengine.

Wenyeviti wa mabaraza ya Ardhi kutoa hukumu kwa Kiswahili
Libya yapata serikali ya mpito