Msanii wa Nigeria, YCEE anayetamba na wimbo wake wa ‘Omo Alhaji anatarajia kutua Dar es Salaam Agosti 28 mwaka huu kwa ajili ya kufanya ziara ya kimuziki akiutambulisha wimbo wake, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kuizunguka Afrika.

Msanii huyo anatarajia kufanya ziara ya vyombo vya habari kwa siku nne (Agosti 29 hadi Septemba 1), ambapo atazitambulisha pia kazi zake nyingine.

“Nina hamu sana ya kukutana na mashabiki wangu wa Tanzania, kwa sababu upendo wanaoniipatia kwenye mitandao ya kijamii ni wa ajabu. Ninafuraha sana kukutana na watu wapya,” alisema YCEE.

YCEE ambaye pia hupenda kushiriki kazi za kijamii, anatarajia kuchangia msaada wake kwa kituo cha ‘Kigamboni Community Center (KCC)’.

Baada ya kutoka Tanzania, Msanii huyo ataelekea nchi jirani za Afrika Mashariki na Afrika Kusini kuendelea na ziara yake ya kulizunguka bara la Afrika.

Majaliwa amwakilisha Rais Magufuli mkutano wa Wakuu wa Nchi TICAD
Jaji Warioba amjibu Kingunge kuhusu UKUTA, “Hili sio tatizo la mtu mmoja”