Ni jambo jema kumshukuru Mungu kwa neema ya upendeleo aliokupa kwani kuna wenye mitihani mizito ya kukosa kiungo muhimu ulichonacho.

Mwanamke aliyetambulika kwa jina la Elmira Knutzen, ameweka mtandaoni kipande cha video cha kusikitisha kinachomuonesha mtoto wake wa kike, Vasiliny aliyezaliwa bila mikono akijifunza kutumia miguu yake kula chakula.

Video hiyo iliyoanzia katika ukurasa wake wa Facebook na kupata umaarufu kwa muda mfupi mitandaoni, inamuonesha mtoto huyo aliyeweka uma katikati ya vidole vyake vya miguu akichota chakula kwenye kibakuli na kujilisha.

Ndani ya wiki moja, video hiyo imeshaangaliwa zaidi ya mara milioni 46. Tumia kila ulichonacho kwa kumtukuza Mungu kwani umepata kwa neema tu.

CUF walia na Polisi, wadai kuna ajenda ya siri dhidi yao
Nicki Minaj amvaa Kanye West kwa alichokiimba kuhusu wanawake