Aliyekuwa Mkurugenzi wa Utendaji wa Klabu ya Simba, Crescentius Magori  amesema kuwa klabu ya Simba siyo mali ya mzee Kilomoni, hivyo hata hati aliyonayo haiwezi kuzuia chochote ndani ya Simba.

Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, ambapo amesema kuwa mzee huyo alikaribishwa tu katika klabu hiyo kama wanachama wengine hivyo yeye siyo mwanzilishi.

Amesema kuwa hawa wazee waliopo Simba kwa sasa hawakuanzisha Simba na walioanzisha wote walishakufa na hawa waliopo nao watakufa, hivyo hakuna mtu mwenye hati miliki na klabu hiyo.

Aidha, Magori amewatoa hofu mashabiki na wapenzi wa Simba kwa kuwataka kumpuuza mzee Kilomoni kwa kile anachakifanya kwani klabu haiathiriki kwa chochote na mambo yote yanaendelea vizuri kama yalivyopangwa.

 

Watendaji kata wakabidhiwa pikipiki
Video: Wakili Manyama atoa ufafanuzi kuhusu sheria ya kodi