Waziri wa Habari, utamaduni, michezo na sanaa, Nape Nnauye amemkabidhi bendera ya Taifa mwanamuziki wa kizazi kipya hapa nchini, Nasibu Abdul (Diamond) kwenda kuiwakilisha Tanzania katika ufunguzi wa mashindano ya AFCON 2017, nchini Gabon ambako amealikwa kwa ajili ya kutumbuiza.

Nape amesema kuwa, kuwepo kwa Diamond kwenye uzinduzi wa michuano hiyo ni kitendo cha kujivunia na kwamba Serikali ikishirikiana na DStv imefanya jitihada kubwa kufanikisha safari ya WCB kuelekea Gabon.

 

Majaliwa ataka miradi inayojengwa iendane na thamani
Waigizaji Marekani kuandamana mara baada ya Trump kuapishwa

Comments

comments