Msanii wa Bongo Movie, Elizabeth Michael amethihirisha noma yake katika uigizaji baada ya kutengeneza Movie inayokwenda kwa jina la ‘Ni Noma’ ambayo kuanzia kesho tarehe 15. July 2016 itaingia sokoni rasmi ikiuzwa katika teknolojia mpya ya Proinbox.

Filamu ya Ni Noma ‘Demu huyu ni Feki’ imetayarishwa na mtayarishaji mahiri kabisa wa filamu za kimataifa kutoka Swahilihood Staford Kihore.

Hii hapa Trailer ya Ni Noma

Sinema ya Ni Noma ‘Demu huyu ni Feki’ imewashirikisha vijana kama Isalito, Baba James, Kulwa Kikumba ‘Dude’, nyota kutoka mradi mkubwa kabisa wa kukuza vipaji wa Tanzania Movie Talent (TMT) ambapo wameonyesha uwezo mkubwa sana katika sinema hiyo.

Ni noma kufanya Mapinduzi ya Filamu Nchini- Lulu
Rais Magufuli amsifu Meya na Wabunge wa Ukawa, wakutana na Dk Tulia