Ofisi ya Taifa ya Takwimu imetoa taarifa ya mfumuko wa bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka na umeongezeka hadi asilimia 5.5 kutoka asilimia 5.2 kwa mwaka jana.
Akitoa taarifa hiyo Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Takwimu, Ephraim Kwesigabo ameeleza kasi ya upandaji wa bei za bidhaa kwa mwaka ulioishia Juni, 2016 imeongezeka ikilinganishwa na bei za Mei mwaka huu.