Viongozi wa Umoja wa Kutetea Katiba ya Wananchi (Ukawa) leo Oktoba 1, 2016 wametoa tamko kuwa hawamtambua aliyekuwa mwenyekiti wa Chama cha Wananchi  (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba na kuongeza kuwa nguvu za kiganga anazotumia haziwezi kufanikisha mambo yake yanayoenda kinyume cha sheria.

Tamko hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe wakati akiongea na waandhishi wa habari katika hoteli ya Protea Courtyard iliyopo Upanga jijini Dar es salaam ambapo ameeleza kuwa Umoja huo unamtambua Julius Mtatiro kama mwenyekiti  wa Chama cha Wananchi (CUF) na Mwenyekiti mwenza wa Ukawa.

 

SimbaYanga: Vurugu zaibuka uwanjani kupinga goli la Tambwe, polisi wapiga mabomu
Diamond amkaribisha Ali Kiba WCB