Kiongozi wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), mkoa wa Kigoma, Augustino Matefu amesema kuwa mbunge wa Kigoma Mjini kupitia Chama Cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe si muadilifu.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa kwasasa ni vyema kujikita katika kumuunga mkono rais Magufuli kwa jitihada zake za kuinua uchumi.

”Huyu Zitto inabidi amuunge mkono Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye anafanya kazi kubwa ya kuinua uchumi wa taifa, aache kupinga kila kitu, maana kwasasa tunasonga mbele kwa kasi,”amesema Matefu

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Desemba 23, 2018
Basata wawakazia Diamond, Ray Vanny kuimba Kenya

Comments

comments