Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Novemba 8, 2016 limeridhia rasmi msimamo wa Serikali wa kutokusaini Mkataba wa ubia wa Uchumi baina ya Nchi za Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Nchi za Ulaya (EU) – (EPA) kwa kuwa hauna manufaa kwa nchi ya Tanzania.

Kwa upande wake Mbunge wa Mwibara (CCM), Kangi Lugola wakati akichangia hoja Bungeni amempongeza  Rais Magufuli kwa kukataa kusaini Mkataba huo kwani ni miongoni mwa Mikataba mibovu kati ya mikataba iliyowahi kuletwa nchini kutoka katika nchi za Ulaya.

“Kama tukikubali kusaini mkataba huu nchi hii itakuwa dampo la bidhaa mbalimbali za ajabu kutoka nje na hivyo kupelekea kushindwa kutimiza dhamira ya nchi ya kuimarisha viwanda vyetu”, alisema Lugola.

Tazama hapa

John Legend azua kizaazaa kwa kumpigia 'debe la mwisho' mmoja kati ya Trump na Clinton
Prof. Mchome: Toeni elimu ya haki za binadamu kwa umma