Wakili wa Kujitegemea, Leonard Manyama amemtaka Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe kuacha kupotosha umma kuhusu ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Prof. Mussa Assad.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na Dar24 Media, ambapo amesema kuwa ufafanuzi uliotolewa na Zitto Kabwe hauna ukweli wowote kwani ripoti hiyo ilikuwa bado haija jadiliwa.

”Si kila kitu kilichoandikwa kwenye ripoti ya CAG ni sahihi, ndio maana ripoti hiyo inatakiwa ijadiliwe kwanza ndio ianze kufanyiwa kazi, na hiki anachokifanya Zitto ni kutaka kutafuta umaarufu wa kisiasa ambao hauna maana yeyote kwa jamii na Watanzania kwa ujumla,”amesema Manyama

 

 

 

Watu 11 wakamatwa, mauaji ya Daktari wa Ebola DRC
RC Chalamila awataka viongozi kuacha unafiki

Comments

comments