Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, George Simbachawene amesema lipo tatizo kubwa la uvamizi kwenye maeneo ya shule za Msingi, Sekondari, Zahanati na maeneo ya masoko, hivyo umefika muda wavamizi hao kuondoka wenyewe au Serikali itawaondoa kwa nguvu kama wasipofanya hivyo kwa wakati waliopewa.

Waziri Simbachawene ameongea hayo leo Oktoba 6, 2016 wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es salaam ambapo ameongeza kuwa ni marufuku kujenga vyumba vya biashara kuzunguka shule na sehemu za kutolea huduma za afya. Bofya hapa kutazama video

Video: Tusiime yapewa siku 14 kulipa faini ya shil. mil.10, uchafuzi wa mazingira
Video: Matembezi ya hisani kuhamasisha uchunguzi wa Saratani kufanyika