Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, January Makamba amesema Sheria ya Usimamizi  wa Mazingira ya mwaka 2004  inapiga marufuku uchafuzi wa mazingira ikiwa ni pamoja na unaotokana na taka za hospitali.

Amesema Kanuni za Taka Hatarishi za mwaka 2009 zinasisitiza utenganishi wa taka mbalimbali  zitokazo kwenye hospitali kwa kuzitibu katika namna ambayo haitaleta athari katika mazingira na afya ya binadamu.

Ameyasema wakati akizungumza na waandishi wa habari leo  na kuongeza kuwa kanuni zinahimiza matumizi ya teknolojia sahihi kama vile matumizi ya vyombo ambavyo huchoma, taka za hospitali na  kuziteketeza kabisa.

”Ofisi yangu imefuatilia na kugundua kuwa taka nyingi za hospitali, taka kutoka katika maduka ya  madawa zilizoisha muda wake zinatupwa ovyo  au kuharibiwa kwa utaratibu usiokubalika kitalaamu. Tumefuatilia na kukuta malundo ya madawa chakavu na vifaa vya hospitali vilivyotumika katika maeneo ya visiwa vya Bongoyo na Mbudya,  madawa chakavu yanatupwa holela katika dampo la Pugu Kinyamwezi.  Hii ni hatari sana kwa mazingira na kwa afya ya binadamu,” – Makamba. Bofya hapa kutazama video

Utafiti: 42% ya wanaume, wanawake Japan ni 'Bikira', Serikali yahaha...
Video: DC Happi azindua mfumo wa wataalamu wa wajasiliamali