Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Kigoma, Agustino Matefu amepokea zaidi ya wanachama 100 kutoka chama cha ACT-Wazalendo.

Katika mkutano huo wa kuwapokea wanachama hao uliofanyika jijini Dar es salaam, wanachama hao wakiwemo madiwani wamesema kuwa, wameamua kukihama chama hicho baada ya kuona kinakosa muelekeo.

“Kama mnavyoona waandishi wa habari, hawa wote siwajui lakini wameamua kuniita ili waweze kujiunga na chama cha mapinduzi CCM, na hizi ni salamu kwa Zitto kwamba 2020 atafute kazi ya kufanya au arudi kwao Kongo,”amesema Matefu.

 

 

 

 

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Desemba 16, 2018
Video: Manispaa ya Kinondoni yawahimiza wasanii kujitokeza na kujisajili TACIP

Comments

comments