Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Innocent Bashungwa amewa Vijana wote wanaopata fursa za kupata mafunzo ya JKT, kuzitumia stadi za kazi na maisha walizozipata kujiajiri na kujitegemea.

Bashungwa ameyasema hayo hii leo Mei 24, 2023 Bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2023/2024 ya Wizara hiyo na kuongeza kuwa JKT imeendelea kuwapatia Vijana mafunzo ya ukakamavu, stadi za kazi, uzalendo na umoja wa kitaifa.

Amesema, “mafunzo yamefanyika kwenye kambi mbalimbali za JKT kupitia Operesheni Jenerali Venance Mabeyo, Vijana 24,458 kwa mujibu wa sheria wamepatiwa mafunzo, kati yao 17,942 wa kiume na 6,516 wa kike.”

Aidha, Bashungwa ameongeza kuwa, Vijana 11,358 wa Kujitolea wamepatiwa mafunzo, kati yao 7,483 ni wa kiume na 3,875 ni wa kike, ili baada ya kumaliza muda wa mafunzo na kuitumikia JKT, waweze kurejea majumbani wakiwa raia wema, wazalendo na wenye uwezo wa kujitegemea na kulilinda Taifa.

Gatoch: Simba SC nimewasikia, njooni tuongee
Iddy Pialali abadilishiwa mpinzani