Beki na nahodha wa Man City, Vincent Kompany hatokuwa sehemu ya kikosi cha klabu hiyo ambacho kesho kitafahamu mbivu na mbichi za kucheza hatua ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya kwa kupambana na mabingwa wa soka kutoka nchini Ufaransa Paris Saint-Germain, katika mchezo wa mkondo wa pili wa hatua ya robo fainali.

Meneja wa Man City, amethibitisha kukosekana kwa Kompany, alipozungumza na waandishi wa habari muda mchache uliopita mjini Machester, kwa kusema beki huyo kutoka nchini Ublegiji bado hajapata utumamu wa mwili licha ya kuanza mazoezi na kikosi cha kwanza.

Amesema alitarajiwa kumtumia katika mchezo huo ambao una umhimu kwake na kwa klabu pia, lakini taarifa alizozipokea kutoka kwenye jopo la matatibu zimemsitishia mipango yake.

Kompany aliumia kiazi cha mguu mwezi uliopita katika mchezo wa ligi kuu ya soka nchini England na alizusha hofu miongoni mwa mashabiki na maafisa wa Man City kufuatia taarifa za awali kueleza huenda angekaa nje ya uwanja hadi mwishoni mwa msimu huu.

Kutokana na maelezo yametolewa na Pellegrini kuhusu beki huyo mwenye umri wa miaka 30, inamaanisha Nicolas Otamendi ataendelea kusimama katika safu ya ulinzi kwa kushirikiana na Eliaquim Mangala.

Otamendi amefanyiwa vipimo na ameonekana kuwa na utimamu wa mwili, baada ya kupata majeraha ya kifundo cha mguu, wakati wa mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya West Brom.

Man City wataingia katika uwanja wao wa nyumbani wa Etihad, huku wakiwa na kumbukumbu ya matokeo ya mabao mawili kwa mawili dhidi ya PSG waliyoyapata jijini Paris nchini Ufaransa juma lililopita.

Endapo watahitaji kusonga mbele, itawalazimu kusaka matokeo ya sare ya bila kufungana ama isiyozidi bao moja ama kusaka ushindi.

Katibu Mkuu Mpya wa Chadema ampima Dk Slaa
Makonda apiga marufuku kuwapa pesa Ombaomba barabarani