Viongozi wa Afrika Mashariki wametangaza mazungumzo ya amani katika juhudi za kurejesha utulivu mashariki mwa DRC, ambako waasi wa M23 walikabiliana na jeshi la serikali, kaskazini mwa mji huo muhimu wa Goma.

Tangazo hilo muhimu la jumuiya ya Afrika Mashariki EAC, linakuja wakati vikosi vya jeshi la Congo vikipambana upya na waasi wa M23 kaskazini mwa mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini, huku taarifa za kijeshi zilisema wanakabiliana na M23 katika kijiji cha Mwaro, kilichoko umbali wa kilomita 20 kaskazini mwa mji huo.

Viongozi wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, EAC.

Waasi hao wa M23, wameibuka hivi karibuni kote katika mkoa wa DRC wa Kivu Kaskazini, wakipata ushindi kadhaa dhidi ya jeshi na kuteka maeneo makubwa ya ardhi na mapema Mei 12, 2022 kundi hilo lilitupa lawama kwa jeshi la Congo kujibu mashambulizi kwa kutumia mabomu na kuua raia 15, wakiwemo watoto wawili.

Waasi wa M23 ambao wana wapiganaji wengi wa kabila wa Watutsi, walijitokeza kwa mara ya kwanza mwaka 2012 walipouteka kwa muda mfupi mji wa Goma kabla ya kusambaratishwa na wakaibuka tena mwishoni mwa 2021, na kuanzisha tena mapambano kwa madai kwamba DRC ilishindwa kutimiza ahadi yake ya kuwajumuishwa jeshini.

Polisi wachunguzwa unyanyasaji washiriki COP27
Picha: NSSF katika Maonesho ya Utalii Karibu Kusini