Tuhuma za usaliti ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) zimewapelekea baadhi ya viongozi waandamizi wa chama hicho mkoani Iringa kufungiwa ndani ya ofisi za jengo hilo kwa kile kilichodaiwa wameshindwa kuchukua hatua dhidi ya wasaliti.

Taarifa kutoka mkoani humo zimeeleza kuwa tukio la kuwafungia ndani viongozi hao limefanywa na baadhi ya vijana wa chama hicho kwa lengo la kumshinikiza Mwenyekiti wa chama hicho, Jesca Msambatavangu kujiuzulu.

Vijana hao walidai kuwa kushindwa kuwachukulia hatua wasaliti na kuwalea ndiko kulikopelekea chama hicho kishindwe kupata ushindi katika jimbo la Iringa Mjini na kupata madiwani wachache. Walishikilia msimamo wakutowafungulia viongozi hao waandamizi licha ya kuombwa na baadhi ya viongozi wa chama hicho waliokuwa nje.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza alifika na polisi na kuwasihi vijana hao kuwafungulia viongozi hao ili waweze kufanya mazungumzo na kufikia muafaka.

Baada ya kuwasihi kwa muda mrefu, vijana hao wakiwa na Mwenyekiti na Katibu Kata wilaya ya Iringa Mjini, Mussa Mbungu walikubali kuwafungulia vijana hao na kuweka masharti kuwa endapo hatua stahiki hazitachukuliwa, zoezi hilo litakuwa endelevu.

Sakata la TBC1: Je wajua ni kosa TV kurusha Tangazo la Biashara kwenye Taarifa ya Habari? Soma hapa
Blatter, Platini watupwa rasmi nje ya soka kwa miaka 8