Sakata la TBC1 kurusha moja kwa moja sherehe ya harusi limeendelea kuwa gumzo mitandaoni huku Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Sanaa, Nape Nnauye akiutaka uongozi wa Shirika hilo la habari la taifa kujieleza.

Zogo hilo mitandaoni limezua mitazamo tofauti huku yakiibuliwa makosa mengine yanayofanywa dhahiri na vyombo vya habari nchini na kugeuzwa kuwa utaratibu wa kawaida unaosaidia kuingiza kipato.

Moja kati ya makosa ambayo hufanywa na televisheni zote nchini ni kurusha matangazo ya biashara wakati wa taarifa za habari.

Dotto Bulendu, Mkurugenzi wa radio SAUT FM iliyoko jijini Mwanza amendika haya kwenye Facebok:

Naona mjadala kuhusu TBC kurusha harusi umekuwa mkubwa sana, makombora kwa TBC ni nonstop, binafsi kabla ya kuwalaumu TBC lazima tusikie upande wao kujua kwa nini waliamua kurusha live harusi?

Kwa nini TBC wanafanya biashara huku ni chombo cha serikali kinachotakiwa kupewa ruzuku? waweza kuta hawapewi pesa za kutosha zaidi ya mishahara ya watumishi, moja ya changamoto kubwa kwa taasisi za serikali ni pesa ya maendeleo, leo sheria ya utangazaji inakataza kurusha matangazo ya biashara kwenye taarifa za habari kwa maana ya news program zote, leo taarifa za habari zote zinadhaminiwa na makampuni ya biashara kinyume na sheria, TCRA na serikali wapo kimya, kuna mambo mengi ya hovyo kuliko hili la Harusi yanaendelea kwenye media.

Waziri Kitwanga Ayakwepa Majina ya Wauza 'Unga'
Viongozi wa CCM wafungiwa ndani Kwa Saa Nne Kuwasaka Wasaliti