Maaskofu hao wa Kanisa Katoliki katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC, wameitisha maandamano ya nchi nzima Desemba 4, 2022 ili kuimulika hatari inayoikabili nchi yao huku wakipaza sauti dhidi ya walichokiita ”unafiki wa jumuiya ya kimataifa” na kutoa wito kwa Wakongomani kupinga mpango wa kuigawa nchi hiyo.

Kauli ya maaskofu hao wa CENCO, inakuja baada ya Mkutano wao maalumu uliofanyika Novemba 7-9, 2022 wiki hii jijini Kinshasa, na kuituhumu Rwanda kuishambulia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na kuongeza kuwa mashambulizi hayo ni mpango wa kuigawa Kongo.

Maaskofu wa Kanisa Katoliki katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC. Picha ya D. Kannah Mukoya/ AFP

Wamesema, “Jumuiya hii imetoa vikwazo kwa makundi yenye kumiliki silaha yakiwemo M23. Lakini haikuviwekea Rwanda wakati  inajua vizuri kama waasi hao wanaungwa mkono na Rwanda. Inamaanisha nini kwani jumuiya ya kimataifa ina uwezo wa kusimamisha vita hivi, kinacholengwa ni nini kama siyo kuigawa nchi yetu.”

Aidha, Maaskofu hao pia walizungumzia suala la kudumisha amani katika nchi yao ambako idadi ya watu wanaofariki inaongezeka kila kukicha kutokana na vita vinavyoendelea mkoani Kivu Kaskazini na kuilaani Jumuiya ya Kimataifa.

Maaskofu wa Jumuiya ya CENCO. Picha ya T. Mukoya/ Reuters

Kupitia umoja huo, Katibu Mkuu wa CENCO Askofu Donatien Tshole amesema, “Kongo ni nchi kubwa, Kongo ni mwanachama wa Umoja wa Mataifa. Kongo inaweza kuwa na imani kwa Umoja wa Mataifa kwa sababu umehamasishwa kuunga mkono juhudi za serikali ya Kongo kuleta utulivu mashariki mwa nchi hii. Mipango mingi inayolenga uthabiti wa nchi hii inaungwa mkono na Umoja wa Mataifa.”

Lakini sio wao tu wanaotoa miito ya raia kuingia mitaani, kwani maandamano mengi yanafanyika hapa nchini katika juhudi za raia kuonyesha hasira zao dhidi ya wanachoamini ni mashambulio ya Rwanda na Uganda kupitia waasi wa M23 ambao Kinshasa inawataja kuwa magaidi.

Dozi laki sita chanjo ya kipindupindu zawasili
Neema yazidi kumwangukia Kijana Majaliwa