Mchezo wa ligi ya nchini Italia (Serie A) kati ya SS Lazio dhidi ya SSC Napoli uliochezwa usiku wa kuamkia hii leo, ulilazimika kuahirishwa baada ya kutokea vitendo vya ubaguzi wa rangi vilivyokuwa vikifanywa na mashabiki wa Lazio kwa beki wa kati kutoka nchini Senegal,  Kalidou Koulibaly.

Ripoti kutoka kwenye mchezo huo zinasema kwamba, kelele kumfananisha beki huyo wa klabu ya SSC Napoli na nyani zilikuwa zikipigwa na mashabiki wa Lazio kutoka kwenye majukwaa, zilipelekea muamuzi kupuliza kipyenga cha kumaliza mchezo huo, uliokuwa umefika dakika ya 68 huku Napoli ikiwa mbele kwa bao 2-0.

Lazio wanaweza wakakumbana na adhabu kubwa ya faini kutokana na tabia iliyofanywa na mashabiki wao.

Senegal defender Kalidou Koulibaly was racially abused by sections of Lazio's home supportKalidou Koulibaly

Meneja wa klabu ya SSC Napoli, Maurizio Sarri amempongeza muamuzi wa mchezo huo, Massimiliano Irrati kwa kuusimamisha mchezo huku akisema anajihisi vibaya kelele za kibaguzi zilizokua zikipigwa kutoka kwa mashabiki wa SS Lazio kwenda kwa Koulibaly.

Koulibaly (behind referee) looks distraught and has to be comforted by Jorginho after suffering racist abuseMuamuzi wa mchezo Massimiliano Irrati

Gonzalo Higuan na Jose Callejon ndio wafungaji wa mabao mawili ya Napoli katika mchezo huo, na kama maamuzi mengine yataamuliwa huenda klabu hiyo ikaendelea kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi ya Serie A, pointi mbili mbele ya mabingwa watetezi Juventus, huku SS Lazio wakiwa wanashika nafasi ya tisa.

Jackson Martinez Auzwa China Akitokea Mjini Madrid
Chelsea Wabanwa Mbavu Na Watford