Wabunge wa Upinzani wameungana na baadhi ya wabunge wa CCM kupinga uamuzi wa Spika wa Bunge kukataa hoja ya kujadili sakata la wanafunzi 7000 wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kuondolewa chuoni ndani ya saa 24.

Hali hiyo ilitokea baada ya Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nasari kusimama na kuomba Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson kusitisha mijadala ya Bunge na kuruhusu Bunge lijadili suala hilo, lakini alikataliwa kwa madai kuwa suala hilo haliwezi kusababisha Bunge kuahirisha mijadala yake.

Hoja ya Nasari iliungwa mkono na wabunge wote wa Upinzani na baadhi ya wabunge wa CCM waliosimama na kupinga kwa kauli moja katazo la Naibu Spika. Hali hiyo ilipelekea Naibu Spika kuahirisha Bunge hadi leo jioni.

Uongozi wa Udom ulitoa tangazo la kuwataka wanafunzi 7000 wanaosoma Stashahada ya ualimu wa Sayansi, Hisabati na Teknolojia kuondoka katika chuo hicho mara moja ndani ya saa 24 kwa madai kuwa ni agizo kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi.

Maambukizi ya vvu kufikia 000 ifikapo 2030!!!
Polisi dar yaingizia Serikali milioni 500 kwa mwezi