Wachezaji Nicolas Wakiro Wadada na Abdallah Kheri Sebo wataukosa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mwadui FC utakaochezwa Kesho Jumamosi (Macho 06), Uwanja wa Mwadui Complex mkoani Shinyanga.

Wawili hao wanaocheza nafasi ya ulinzi wataukosa mchezo huo muhimu kwa Azam FC, kufuatia majeraha walioyapata mjini Bukoba wakiwa kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar, uliomalizika kwa wenyeji kufungwa mabao mawili kwa moja.

Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino ya Azam FC Thabit Zakaria ‘Zaka Zakazi’ imeeleza kuwa, wachezaji hao wanaendelea vizuri.

Azam FC tayari imeshawasili Shinyanga, ikitokea Bukoba mkoani Kagera tayari kwa mchezo huo ambao unasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa pande zote mbili.

Baada ya kuwasili, jana jioni Azam FC ilifanya mazoezi kwenye uwanja wa Fresho Complex na leo itafanya mazoezi Mwadui Complex saa 10 jioni.

Azam FC inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na alama 49 baada ya kucheza michezo 22, huku Mwadui FC inayonolewa na kocha mzawa Amri Said ikiwa nafasi ya 18 zilizopatikana kwenye michezo 22 waliocheza mpaka sasa.

Manara: Tupo tayari kuikabili Al Merrikh
Trump kufunguliwa tena YouTube