Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Nchini (HELSB),imesema kuwa itaanza kupita nyumba nyumba, nyumba za ibada  na kwenye sherehe ili kuweza kubaini na kuwakamata wadaiwa sugu wa mikopo ambaao hawajawasilisha taarifa zao na kurejesha mikopo hadi sasa.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo, Abdul-Razaq Badru alipokuwa akiongea na waandishi wa habari, amesema kuwa  tangu watoe notisi  kwa wadaiwa hao na kuwaongezea wiki mbili, mwitikio umekuwa ni mkubwa zaidi na kuwezesha kukusanya kiasi kikubwa cha fedha.

“Wiki tatu zilizopita tulitoa ofa kwa wadaiwa, tulianza na wiki nne tukaongeza nyingine mbili, wengi walijitokeza kurejesha kiasi kikubwa cha mkopo, tunaomba ambao bado hawajalipa walipe kabla ya muda wa nyongeza kuisha, hiari ikipita tutapita nyumba kwa nyumba, nyumba za ibaada na kwenye sherehe, naamiini tutawakamata” amesema Badru.

Hata hivyo amesema kuwa wadaiwa wa mikopo 42,700 kati ya 142,000 walijitokeza kulipa fedha hizo tangu Bodi itoe notisi ya mwezi mmoja na kwamba wanufaika walio kwenye mfumo rasmi wa ajira watakatwa asilimia 15 na wasio katika mfumo huo watakatwa  asilimia 10 ya kipato chao.

Bodi ya mikopo kuwasaka wadaiwa nyumba kwa nyumba, kwenye sherehe
Ndoto ya Lema kuwa nje ya gereza mwaka huu yayeyuka