Wafanyakazi wa Clouds Media Group ambao walikuwa wanatokea Bukoba kwenye mazishi ya aliyekuwa mkurugenzi wa vipindi, Ruge Mutahaba wamepata ajali nje kidogo ya Jiji la Dodoma wakati wa safari ya kuridi jijini Dar es salaam.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Clouds Media imesema kuwa, wafanyakazi hao wamepelekwa hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu na vipimo zaidi.

“Tunasikitika kuwataarifu kuwa sehemu ya timu yetu ya production (Watu 6) iliyokuwa ikitokea msibani Bukoba kurejea jijini Dar es Salaam imepata ajali ya gari maeneo ya nje kidogo ya Dodoma, tunamshukuru Mungu hakuna aliyepata madhara makubwa kutokana na ajali hiyo, Pia tunatoa shukrani za dhati kwa mbunge wa jimbo la Dodoma mjini, Anthony Mavunde kwa msaada wa haraka aliowapatia vijana wetu ambao kwa sasa wanapatiwa matibabu na vipimo zaidi Jijini Dodoma.”imesema taarifa hiyo

 

 

 

DAR 24 INATOA POLE KWA WAFANYAKAZI WOTE WA CLOUDS MEDIA.

Korea Kaskazini yadaiwa kujenga upya vinu vya nyuklia
Breaking News: Mwalimu ahukumiwa kunyongwa hadi kufa

Comments

comments