Serikali ya Kenya imetangaza msako dhidi ya raia wa kigeni walio nchini humo bila vibali maalumu.

Hali hii imekuja baada ya hofu kuzuka juu ya ongezeko la makundi ya raia wa kigeni wengi wao kutoka bara Asia ambao wameonekana katika maeneo ya makazi jijini Nairobi.

Takwimu iliyotolewa na wizara ya mambo ya ndani zinaonesha kuwa zaidi ya raia wa kigeni 20,000 wameinga nchini tangu mwezi Juni na karibu 8,000 kati yao wameondoka.

Katibu katika Wizara ya Mambo ya ndani nchini humo Karanja Kibicho, amesema wageni hao wako njiani kuelekea Saudi Arabia kwa kazi.

Saudi Arabia imejumuisha nchi kadhaa za Asia katika orodha nyekundu, ambayo ilibuniwa kuzuia kusambazwa kwa virusi vya corona.

Bw. Kibicho hata hivyo amesema Kenya inakabiliwa na tishio la kuenea zaidi kwa virusi vya Covid-19 ndio sababu ya kutaka kudhibiti idadi ya watu wanaopita nchini hiyo.

Raia hao wa kigeni wanaishi Nairobi na jimbo jirani la Machakos.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, October 1, 2021
Rais Samia aongoza wananchi kuaga mwili wa Hayati Ole Nasha